Athari za za kibukusu kama lugha ya kwanza katika kujifunza lugha ya pili Kiswahili
Abstract
Napenda kumshukuru Maulana kwa wema na ukuu wake maishani mwangu. Ni Mungu aliye na rehema na nehema zisokuwa na kipimo maishani mwangu kwani kanijalia uhai na ufahamu ulioniwezesha kukamisha kazi hii.Ninamshukuru Baba ya William Ochieng' na mama yangu Joice Nasike kwa mashauri, na maombi yao kuona kuwa nafanikiwa katika maisha haya. Ni wazazi ambao walinitia moyo pale nilipoona kuwa nimeshindwa. Mwenyezi Mungu awape maisha marefu ili muweze kukula matunda ya jasho lenu.
Shukrani za pekee nampa dada yangu Becky. Amelia wa manufaa sana kwa masomo yangu. Alijinyima ili anilipie karo ya chuo kikuu. Mungu akuongezee dada. Siezi msahau mpenzi wangu Kevin Wanjala. Amelia rafiki wa karibu sana kwangu na alinitia moyo kila mara akiniombea mema kimasomo. Ubarikiwe sana ndugu Kevin.
Shukrani za pekee ninampa msimamizi wangu mpendwa Bi. Assimwe Caroline kwa kutumia muda wake kunitia moyo kimasomo wakati nilionekana kukata tamaa. Kichwa ya upungufu niyokuwa nayo aliweza kunivumilia, akapitia kazi yangu akaisahihisha na kunielekeza vilivyo kuhakikisha kuwa ni kazi nzuri na yakunisaidia nifuzu vyema. Mungu amtende mema huyu msimamizi.
Pia nawashukuru marafiki zangu kama Moraa Janet, Obwona Simon Peter na wengine wote kwa kusimama nami na kuhakikisha nifanyacho chuoni ndicho kilichonipeleka huko. Mungu awape mafanikio maishani mwenu. Nawapenda Sana.